Usinikemee Bwana

Usinikemee Bwana
Performed by-
CategoryZaburi
Views2,473

Usinikemee Bwana Lyrics

  1. Usinikemee Bwana kwa hasira yako
    Uniadhibu Bwana kwa ghadhabu yako,
    Unihurumie ee Bwana Mungu wangu
    Uniponye Bwana mwenyezi Mungu
    Kwani mimi Bwana mimi ni dhaifu,
    natetemeka mpaka mifupani
    {[b:] Ewe mwenyezi Mungu) –
    Ukawie mpaka lini Bwana unigeukie uniokoe}*2

  2. Na nafsi yangu imefadhaika sana,
    wewe Bwana mpaka lini
    Bwana urudi uiokoe nafsi yangu
    uniokoe mimi Bwana
  3. Nimechoka kwa kuugua kwangu nateseka kitandani
    Kila usiku nalilowesha Godoro langu
    kwa machozi yangu
  4. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu ya dunia
    Na kuchakaa kwa sababu ya hao
    wanaoniudhi mimi Bwana