Utukufu Juu Kwa Mungu

Utukufu Juu Kwa Mungu
Performed by-
CategoryTBA
Views15,841

Utukufu Juu Kwa Mungu Lyrics

  1. Utukufu juu kwa Mungu, na amani duniani
    Kwa watu wenye mapenzi, kwa
    watu wenye mapenzi mema
    Wenye mapenzi mema

    Tunakusifu [Bwana] tunakuheshimu
    Tunakuabudu tunakuabudu
    Bwana tunakutukuza

  2. Tunakushukuru Mungu kwa ajili
    Ya utukufu wako mkuu
    E Bwana ndiwe Mungu Mfalme wa milele
  3. E Mwenyezi Mungu Baba Ewe Bwana Yesu Kristu
    Mwana wa pekee wa Mungu,
    Mwanakondoo wa Mungu, Mwana wake Baba
  4. Unayeondoa dhambi, dhambi zote za dunia
    Bwana utuhurumie, Bwana utuhurumie
    Pokea ombi letu
  5. Mwenye kuketi kuume kuume kwake Mungu Baba
    Bwana utuhurumie, pekee yako Bwana
    Ndiwe mtakatifu
  6. Pekee yako ndiwe Bwana, pekee yako mkuu
    Ee Bwana Yesu Kristu, na Roho Mtakatifu
    Milele na milele