Watu Hawatalingana Lyrics

WATU HAWATALINGANA

@ Fr. A. Msigwa

 1. {Watu hawatalingana (daima), watatofautiana
  (nayo ni) makusudi yake Mungu, jina lake litukuzwe } *3

  { Sote tumeumbika tulivyo (kadiri) ya mapenzi yake Mungu
  Ili utukufu wake Mungu (Mwenyezi) ujulikane kwa wote } *2

 2. Kweli wanadamu wote (hakika) tumeumbwa kwa udongo
  (hivyo) asili yetu ni moja, tumetoka mavumbini
 3. Wapo walio wanyonge (lakini), pia wapo wenye nguvu
  (kusudi) Mungu kawaumba hivyo, ili wahudumiane
 4. Wengine kawabariki (sana), amewajalia mali
  (lakini) wengine amewashusha, wamekuwa hohe hahe.
 5. Wale walio tajiri (kamwe), wasiwanyime fukara
  (kwani) maskini wahitaji, huruma ya matajiri
 6. Wote tu wana wa Mungu (hivyo) tuonyeshane upendo
  (ili) Mungu wetu atukuzwe, sasa na hata milele.
Watu Hawatalingana
COMPOSERFr. A. Msigwa
CHOIRKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
ALBUMWatu Hawalingani
CATEGORYTafakari


Baadhi ya kwaya ambazo zimerekodi wimbo huu ni
* Kwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha (Watu Hawalingani album)
* Kwaya ya Mt. Vincenti Palloti Makiungu Dsm (Wema Mkamilifu album)
* Kwaya ya Mt. Paulo, Chuo Kikuu cha Nairobi (Ikatetemeka Nchi album)
 • Comments