Yesu Alia Msalabani

Yesu Alia Msalabani
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Yesu Alia Msalabani Lyrics

 1. Yesu alia msalabani. Asikitika juu ya dhambi zetu
  Asulubiowa asiyekosa kwamba yeye ni mosaji

  Ee mwanadamu lipi ambalo linalonipasa kuwatendea
  Ambalo sikuwatendeeni, hata ikanipasa msalaba

 2. Magonjwa yote aliyaponya, wafu nao aliwafufua
  Kundi la watu aliwaponya, lipi alilokosa
 3. Watu wa Mungu Bwana alia asikitika juu ya dhambi zenu
  Asulubiwa asiyekosa kwamba ni mkosaji
 4. Wana wa Mungu, Bwana alia, asema nyinyi mwamsulubisha,
  Msipobeba misalaba yenu kwani nyinyi m wakosaji
 5. Tazama Bwana akulilia, akuita ndipo akuokoe
  Tazama haya mapenzi yake Bwana hayana mwisho