Zawadi Tosha

Zawadi Tosha
Performed bySt. Francis of Assisi Kariobangi
AlbumZawadi Tosha
CategoryThanksgiving / Shukrani
Views17,030

Zawadi Tosha Lyrics

  1. Nimetunukiwa tuzo lenye thamani
    Nimeletewa zawadi toka mbinguni
    Nimejishindia Mwana wa Mungu
    Nimepewa Yesu zawadi tosha

  2. Ninashangilia naimba kwa furaha
    Ninarukaruka nacheza kwa furaha
    Napiga makofi na vigelegele
    Nimempata Yesu tuzo la ajabu (mimi)
  3. Ninakushukuru ee Mungu Baba yetu
    Nasema asante kwa mema yako yote
    Napiga filimbi, ngoma na kayamba
    Nimejishindia Bwana wa mabwana
  4. Nikiwa na Yesu, magonjwa yamepona
    Nikiwa na Yesu mashaka yamekwisha
    Yesu kiongozi, Yesu Jemedari
    Yesu mchungaji, Yesu mambo yote
  5. Maisha marefu ni tuzo nimetuzwa
    Uzima milele nimeshaahidiwa
    Mbinguni kwa Baba nitakaribishwa
    Nitaishi vyema siku zangu zote