Tumuogope Mungu

Tumuogope Mungu
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumRamani ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerE. F. Jissu
Musical Notes
Time Signature6
16
Music KeyG Major
NotesOpen PDF

Tumuogope Mungu Lyrics

{ Ni nani mwanadamu mwenye nguvu kuliko Mungu (hakuna) } *2
Ajitokeze mbele za watu tumuone, hakuna
Iyelele iyele, iyelele iyele - hakuna *4
Ni Mungu tu awezaye yote hivyo tumwogope

 1. Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
  Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
  Akipanga uwe padri, utakuwa wewe padri
  Akipanga we mtawa, utakuwa we mtawa, muogope Mungu
 2. Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
  Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
  Akipanga uwe raisi, utakuwa we rais
  Akipanga uwe waziri, basi wewe ni waziri, muogope Mungu
 3. Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
  Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
  Akipanga uwe mbunge, basi wewe ni mbunge
  Akipanga uwe balozi, utakuwa we balozi, muogope Mungu
 4. Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
  Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
  Akipanga uwe tajiri, basi wewe ni tajiri
  Akipanga uwe maskini, utakuwa maskini, muogope Mungu
 5. Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
  Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
  Akipanga kukurudisha, mavumbini utarudi
  Analopanga Mwenyezi, daima halipingiki, muogope Mungu