Majukumu Katika Familia

Majukumu Katika Familia
Alt TitleBaba Mama na Watoto
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumIkulu ya Mbinguni
CategoryFamilia
ComposerT. B. Pamera

Majukumu Katika Familia Lyrics

Baba mama na watoto wao ni familia kamili
Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu
Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani
Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake

Mama awe katekista, na baba awe padre
Mama awe katekista, na baba awe padre
{Watoto wawe ubao[ubao] kufundishia wengine
Ili wengineo wajifunze, kuishi maisha mema} *2

 1. Mama awe katekista maana yeye ndiye mwalimu[yeye],
  Kwa kuwa ana huruma[sana] na ni mlezi wa watoto
  Awafundishe mema yote, upendo sala na bidii[ya kazi]
  Na kuwafundisha nidhamu kwa wenyewe na kwa wengine
 2. Baba yeye awe padre, tena yeye ndiye mchungaji[mwema]
  Ashirikiane naye mama, watoto wao kuwalea
  Awe mwelekezaji pale watoto wanapopotoka [warudishwe]
  Ili waweze kujenga familia iliyo bora
 3. Watoto wawe ubao ubao, kufundishia wengine[waige]
  Kwa tabia zao nzuri na uadilifu mwema
  Watakuwa ni mfano bora na kielelezo sawia [cha kuigwa]
  Hiyo ndiyo familia ya kumpendeza Mungu

  Baba mama na watoto wao ni familia kamili
  Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu
  Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani
  Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake