Baba Mama na Watoto

Baba Mama na Watoto
ChoirSt. Cecilia Zimmerman
AlbumNitayasimulia Matendo (Vol 6)
CategoryFamilia
ComposerT. B. Pamera

Baba Mama na Watoto Lyrics

 1. Baba mama na watoto wao ni familia kamili
  Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu
  Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani
  Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake

  Mama awe katekista, na baba awe padre
  Mama awe katekista, na baba awe padre
  {Watoto wawe ubao[ubao] kufundishia wengine
  Ili wengineo wajifunze, kuishi maisha mema} *2

 2. Mama awe katekista maana yeye ndiye mwalimu
  Kwa kuwa ana huruma na ni mlezi wa watoto
  Awafundishe mema yote, upendo sala na bidii
  Na kuwafundisha nidhamu kwa wenyewe na kwa wengine
 3. Baba yeye awe padre, tena yeye ndiye mchungaji
  Ashirikiane naye mama, watoto wao kuwalea
  Awe mwelekezaji pale watoto wanapopotoka
  Ili waweze kujenga familia iliyo bora
 4. Watoto wawe ubao ubao, kufundishia wengine
  Kwa tabia zao nzuri na uadilifu mwema
  Watakuwa ni mfano bora na kielelezo sawia
  Hiyo ndiyo familia ya kumpendeza Mungu

  Baba mama na watoto wao ni familia kamili
  Na hawa wote ni muhimu, kujenga kanisa la Yesu
  Katika kujenga Kanisa la Yesu ujenzi huanza nyumbani
  Na kupeana majukumu, kila mmoja na lake