Ninainua Mikono

Ninainua Mikono
ChoirKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumKidole Juu (Vol 23)
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerA. Sulla

Ninainua Mikono Lyrics

  1. Ninainua mikono kukutukuza Mungu wangu (mwema)
    Ninapiga na makofi kushangilia uwezo wako
    Wewe Mungu ni mwema (kwa wote)
    Huruma yako ni ya mile-le
    Enzi ufalme ni wako milele yote
    Wewe Mungu ni mwema (kwa wote)
    Ukuu wako ni wa mile-le
    Tunakushangilia kwa nyimbo za sha-ngwe

  2. Unatulinda watubariki sisi wanao
    Neema tele watujalia sisi wanano
    Twakushangilia tukiusifu ukuu wako *2
  3. Ajali za kutisha Bwana umetulinda vyema
    Na vifo vya kutisha Bwana umetulinda vyote
    Ni wewe Baba wajua yote
    Kwani hakuna zaidi ya-ko
  4. Tunaimba kwa furaha tukisifu
    Utukufu wako Mungu wetu
    Tunashangilia ukuu na upendo wako