Jina la Yesu Lafanya Mambo

Jina la Yesu Lafanya Mambo
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumRamani ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerC. A. L. Ndomelo

Jina la Yesu Lafanya Mambo Lyrics

Aeeh! Njooni muone - muone
Njooni muone - muone
Njooni muone Jina la Yesu - aeh!
{Linafanya mambo - aa aah!
Linafanya mambo - Jina la Yesu
Lafanya mambo makuu sana} *2

 1. Kwa jina la Yesu pepo wanakimbia
  Kwa jina la Yesu wagonjwa wanapona
  Kwa jina la Yesu viwete wanatembea
  Kwa jina la Yesu vipofu wanaona
 2. Kwa jina la Yesu mabubu wanaongea
  Nao viziwi wana wanakusikia
  Kwa jina la Yesu waganga wanaokoka
  Kwa jina la Yesu dhambi wanazitubu
 3. Kwa jina la Yesu waongo wanaokoka
  Kwa jina la Yesu na wezi wanatubu
  Kwa jina la Yesu wazinzi wanaokoka
  Kwa jina la Yesu Mbinguni wataenda