Hawa Ndio Wanaotapatapa

Hawa Ndio Wanaotapatapa
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumIkulu ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerM. Z. Yohana

Hawa Ndio Wanaotapatapa Lyrics

 1. Hawa ndio wale wasiomkumbuka Mungu
  Ndio wale wasiomtumaini Mungu
  Wanataka maisha ya mkato pasipo kutoka jasho
  Hutamani visivyo vyao viwe vyao
  Tegemeo lao ni kwa waganga ambapo hupewa dumba
  Ili wapate kudhulumu vya wenzao
 2. Hawa ndio wale wanaotapatapa ovyo
  Ndio wale wasiomtumaini Mungu
  Kila siku ni kiguu na njia eti wasaka pesa
  Hata kukumbuka kusali hawataki
  Wamesahau ya kwamba Mwenyezi ndiye mgawa vyote
  Na ndiye mpaji wa vyote kwa wanawe
 3. Hawa ndio wale wanaomkufuru Mungu
  Ndio wanaochezea Jina lake Mungu
  Wanaishi maisha ya uzinzi pasipo kufunga ndoa
  Na maisha yao hujaa machungu mengi
  Wengine wanaharibu miili eti wawe warembo
  Kana kwamba Mungu hakuwaumba vizuri
 4. Hawa ndio wale wanaomdhihaki Mungu
  Ndio wale wasioheshimu uhai wao
  Wanatumia vibaya miili yao kwa ukahaba
  Eti ili wajipatie kitu kidogo
  Wengine wanavyolegeza ndoa sababu ya nyumba ndogo
  Na kuziacha familia zikiteseka
 5. Hawa ndio wale wanaompendeza Mungu
  Ndio wale wanaoshika njia zake Mungu
  Wale walioyatoa maisha yao kuwa sadaka
  Kwa kumtumikia Mungu kwa undani
  Wanaouthamini uhai wao pia na majirani zao
  Wakisaidiana vyema na kupendana