Ingawa Napendeza Lyrics

INGAWA NAPENDEZA

@ Gerdian Rweikiza

Ingawa mimi napendeza, Ingawa wewe wapendeza
Wapendeza machoni pa watu, kupendeza si kitu
Ingawa mimi najipamba, Ingawa wewe wajipamba
Kujipamba kwa mwili si kitu, kujipamba si kitu

Kujipamba kwa imani bila matendo ni bure
Wajidanganya tu
Kujipamba kwa mavazi bila matendo ni bure
Twajidanganya tu

Uzuri wa uso wako - bila Mungu ni bure
Wingi wa mali yako - bila Mungu ni bure
Uzuri watoka kwa Mungu, mali yatoka kwa Mungu
Na majivuno yote, bila Mungu ni bure
Kumbuka kila mtu, kaumbwa kwa jinsiye

 1. Wengi wajisifia kwa maneno ya watu
  Wanapakwa kila kona kwa maneno mazuri
  Bila kufikiria na wewe wajiona mzuri
  Mpaka kufikia kusahau maagano yake
  Kwa kusifiwasifiwa
 2. Uzuri ulio nao mshukuru Mungu
  Mali uliyo nayo mshukuru Mungu
  Uzuri ni talanta toka kwa Mungu
  Tumia uzuri wako kumshukuru Mwenyezi
Ingawa Napendeza
COMPOSERGerdian Rweikiza
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMMaajabu ya Mungu
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYG Major
TIME SIGNATURE2
4
NOTES Open PDF
 • Comments