Login | Register

Sauti za Kuimba

Nyota ya Bahari Lyrics

NYOTA YA BAHARI

@ Alfred Ossonga

 1. Bara na bahari furahini sana
  Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni
  Bara na bahari furahini sana
  Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni

  Tumemulikwa na nyota ya bahari
  Bikira daima (mulika) mulika nyoyo zetu
  Tumeona leo mwangaza wa kweli
  Somo wa kanisa (mulika) mulika njia zetu
  {(Mama) Mama tuombee, mama tuongoze
  Kwa mwanao Yesu, kule uwinguni } *2

 2. Pendo lako mama, limetuvutia
  Tunatangaza sifa zako kwa nyimbo
  Bara shangilia, bahari ivume
  Tumsifu mama, mama wa Maulana
 3. Piga tarumbeta, pigeni mluzi
  Imbeni wimbo wa mama wa Mulungu
  Chezeni pamoja, ruka juu juu
  Mama wa Yesu afurahi Mbinguni
 4. Mama wa Mwokozi, Malkia wa Mbingu
  Mwanga anamu somo wa kwaya yetu
  Uliyekingiwa dhambi ya asili
  Daraja letu tuendao Mbinguni
 5. Nyota za angani zamulika nchi
  Mama Maria anamulika nyoyo
  Usiku mchana anatuangaza
  Tunatembea na nuru siku zote
Nyota ya Bahari
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIROur Lady(Star of the Sea) Kenya Navy
ALBUMTumeandamana
CATEGORYBikira Maria
 • Comments