Waumini Simameni

Waumini Simameni
Performed bySt. Mary's Ongata Rongai
AlbumYesu Nakushukuru
CategoryInjili na Miito (Gospel)
ComposerOchieng Odongo
Views7,658

Waumini Simameni Lyrics

  1. Waumini simameni - tupeleke neno lake
    Neno lake Bwana Mungu - ni nuru ya ulimwengu *2

    Tulisome kweli (kweli kweli)
    Tulihubiri sana(biri sana)
    Tulisambaze kote na tulifundishe kweli

    Tulisome kweli (kweli kweli)
    Tulihubiri sana(biri sana)
    Tulisambaze kote na tulifundishe

  2. Ni neno la Bibilia - kutoka kwa Mungu Baba
    Anena kwa kinywa chake - na kwa maandiko yake *2
  3. Ni dawa ya mioyo yetu - tulizo kwa watu wote
    Tulipokeeni leo - tupate kunusurika *2
  4. Tuchezeni kwa furaha - nderemo na kwa vifijo
    Kwa ngoma na tarumbeta - kayamba hata vinanda
  5. Milima iyumbeyumbe - miti na ichezecheze
    Bahari ivume sana - mito ipige makofi *2