Pilka Pilka

Pilka Pilka
ChoirChrist The King Bungoma
AlbumPilka Pilka
CategoryTafakari
ComposerOchieng Odongo

Pilka Pilka Lyrics

1. Pilka pilka kila siku watu wa dunia
Wanahangaika kutafuta mali za dunia
Asubuhi ni msongamano, mchana vilevile
Usiku shughuli zafanyika kama kawaida

Tafuteni kwanza ufalme ule wa mbinguni
Na hayo mengine (hakika) mtazidishiwa
{Yeye Mungu (Mwenyezi) mtetezi (ajabu)
Mkiamini atawashughilikia } * 2

2. Pilika pilika watu wengi kutafuta elimu
Hawakumbuki kwamba Yesu ni mwalimu tosha
Ajali nyingi barabarani zinafanyika kwetu
Tumesahau kwamba Yesu ni dereva tosha

3. Pilika pilika twatafuta hospitali kubwa
Huku daktari mkuu ni Mungu wa majeshi
Watu watafuta waganga ili wapate mali
Bali Mungu wa mbinguni ndiye mmliki wa vyote

4. Pilika pilika tunawaza usiku na mchana
Vile tutakula vizuri na kuvaa vizuri
Kwani ndege wale wa angani wanalishwa na nani
Kama siyo Mungu wa mbinguni basi huyo nani

5. Pilika pilika wenzangu tumuelekee Mungu
Tusifadhaike bali tuwe na matumaini
Atatujalia mema mengi tukiwa duniani
Mwisho tutafurahi na Yesu kule juu mbinguni

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442