Login | Register

Sauti za Kuimba

Bwana Mungu Tunakuja Lyrics

BWANA MUNGU TUNAKUJA

Bwana Mungu tunakuja mbele zako
Tunakuja leo na zawadi zetu
Zipokee zibariki ziwe za kupendeza

 1. Upokee mkate wetu toka ngano ya nchi hii
  Upokee divai yetu toka tunda la mzabibu
 2. Mazao ya mashamba tunaleta mbele zako
  Nazo fedha za mifuko twaomba uzipokee
 3. Maisha na matendo yetu tunayaleta mbele zako
  Roho zetu zenye toba twaomba uzipokee
 4. Tuhurumie si wakosefu tunakuja mbele zako
  Tuletee baraka zako kwetu sisi wenye dhambi
Bwana Mungu Tunakuja
CHOIR
CATEGORYOffertory/Sadaka
 • Comments