Hiki ni Chakula kwa Wote

Hiki ni Chakula kwa Wote
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)

Hiki ni Chakula kwa Wote Lyrics

Hiki ni chakula kwa wote wampendao
Mkate na divai ni chakula cha Roho
Wanyofu wa moyo twendeni tukampokee
Tupate uzima wa milele na milele

 1. Bwana Yesu alhamisi kuu kajitolea,
  Mwili na damu yake ziwe kiburudisho
  Akatuamuru tukipenda kumkumbuka,
  Mwili na damu ni ishara ya penzi lake
 2. Alaye mwili na kunywa damu asema Bwana
  Aishi ndani yangu na mimi ndani yake
  Yeye ni rafiki yangu na nitamfufua,
  Nitaandamana naye safarini mwake
 3. Alaye mwili wa Yesu na kuinywa damu,
  Bila stahili ana hukumu ya milele
  Tujitakase kabla ya kula karamuyo,
  Kitubio ni sakramenti ya mapatano
 4. Ee Yesu nipe neema ya kukupokea,
  Unipe nguvu ya kuweza kujitakasa
  Unijalie kukupenda na moyo wote,
  Mwishowe nishiriki karamu ya Mbinguni