Login | Register

Sauti za Kuimba

Kwako Bwana Zinatoka Sifa Zangu Lyrics

KWAKO BWANA ZINATOKA SIFA ZANGU

@ John Mgandu

Kwako Bwana zinatoka sifa zangu (sifa zangu) * 4
Katika katika kusanyiko katika kusanyiko kubwa
Aleluya aleluya aleluya

 1. Nitaziondoa nadhiri zangu,
  Mbele ya wamchao * 2
  Wapole watakula na kushiba,
  Wamtafutao Bwana wataamsifu
 2. Miisho yote ya dunia itakumbukwa
  Na watu watamrejea Bwana *2
  Jamaa zote za mataifa watamsujudia,
  Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu
 3. Zitasimuliwa habari za Bwana
  kwa kizazi kitakachokuja *2
  Nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake
  Ya kwamba ndiye aliyefanya ndiye aliyefanya
Kwako Bwana Zinatoka Sifa Zangu
COMPOSERJohn Mgandu
CHOIRSt. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE3
8
NOTES Open PDF


Umerekodiwa na kwaya kadhaa pamoja na
* Kwaya ya Familia Takatifu, Kanisa Kuu la Mtakatifu Yusufu, Jimbo la Dar-es-Salaam
* Kwaya ya Bikira Maria Mama wa Mateso Saba Babati Manyara Arusha
na nyinginezo
 • Comments