Tujongee Mbele ya Meza

Tujongee Mbele ya Meza
Performed byMoyo Safi (Unga Ltd)
AlbumNikupe Nini Mungu Wangu
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerJohn Mgandu
Views5,267

Tujongee Mbele ya Meza Lyrics

  1. Tujongee mbele ya meza yake Bwana
    {
    |s|t| tukale chakula cha uzima,
    tukale chakula cha uzima,
    Bwana ametuandalia
    |a/b| tukale chakula cha uzima cha uzima } * 2

  2. Chakula kiko tayari, Bwana ametuandalia
    Anatukaribisha twende mezani, kwa chakula cha uzima
  3. Hiki ni chakula kweli, kinashibisha roho zetu
    Chakula hiki ni mwili na damu, ya Bwana wetu Yesu
  4. Hiki ni chakula kweli, kinachotoka mbinguni
    Atakayekula chakula hiki, ataishi milele
  5. Damu yangu ni kinywaji kweli, Yesu ametuandalia
    Atakayekunywa damu yangu, anao uzima wa milele