Yumo Humu Mwokozi

Yumo Humu Mwokozi
Alt TitleKaramuni Kwa Maringo
ChoirMbeya
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerBernard Mukasa
Musical Notes
Time Signature2
4
Music KeyA Major
NotesOpen PDF

Yumo Humu Mwokozi Lyrics

 1. Yumo humu, Mwokozi Yesu,
  Kwenye mzabibu, na ngano tamu
  Ni mpole ni mwema ni uzima

  { Waumini (haya), simameni,
  Polepole (tena), kwa imani,
  Jongeeni karamuni (mpate)
  mpate kumwonja Mwokozi Yesu } *2
 2. Ekaristi ni jina lake,
  Pamoja nasi, Mungu mwenyewe,
  Ndani yetu nasi ndani yake
 3. Alitoa, jioni ile,
  Kwa kumbukumbu, yake milele,
  Tule tunywe wote tuokoke6.
 4. Tugeuze, maisha yetu,
  Yakafanane, na meza hii
  Huruma, upendo msamaha

  * * *
 5. Alisema, twaeni mle,
  Twaeni mnywe kwa ukumbusho
  Ni mpole, ni mwema, ni mzima
 6. Ekaristi, katuachia,
  Chakula bora, tufike kwake,
  Ni mpole, ni mwema, ni mzima