Login | Register

Sauti za Kuimba

Nakushukuru Baba Lyrics

NAKUSHUKURU BABA

@ Alfred Ossonga

 1. Nakushukuru Baba (shukuru), Baba Mwenyezi Mungu
  Mwenyezi kwa kuwa umeniumba
  Nakushukuru Baba (shukuru), Baba Mwenyezi Mungu
  Mwenyezi kwa kuwa umeniumba

  Nitakulipa nini ee Mungu, wangu cha kukupendeza wewe
  Baba mimi sina kitu chochote
  Cha kulinganisha na ukarimu wako
  Maombi yangu uyapokee, na dua zangu zikufikie
  Kwa huruma yako Baba nisamehe
  Mimi kwa makosa niliyoyatenda
  Tafadhali Baba uniongezee siku nyingi ili nikutumikie

 2. Nakutukuza Baba (tukuza), wewe ni ngome yangu
  Ngome yangu ndiwe unayenilinda
  Pokea sifa Baba (pokea) sifa ni zako wewe,
  zako wewe Baba Mwenyezi Mungu
 3. Nakuabudu Baba (abudu), Baba Mlinzi wangu -
  Mlinzi kwa kuwa wewe ni mwema
  Uniongoze Baba (ongoze), katika kweli yako,
  Kweli yako nifanye mapenzi yako
 4. Bwana nifanye mimi (nifanye), chombo cha kazi yako
  kazi yako nikutumikie wewe
  Pasipo na amani (pasipo), pasipo na upendo,
  upendo nitangaze Jina lako
 5. Usiniache Baba (ee Baba), uwe nami daima
  Daima katika maisha yangu,
  Nikufuate wewe (fuate), daima siku zote,
  siku zote milele hata milele
Nakushukuru Baba
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments