Ni Mungu Mkuu

Ni Mungu Mkuu
ChoirSt. Kizito Makuburi
AlbumNyumba ya Roho
CategoryGeneral
ComposerBernard Mukasa

Ni Mungu Mkuu Lyrics

 • Ni Mungu mkuu *3 ni Mungu wa ushindi
  Ni Mungu mkuu *3 ni Mungu wa uweza
  Ni Mungu mkuu *3 ni Mungu wa ushindi
  Ni Mungu mkuu uuu mkuu
  Ni Mungu mkuu ni Mungu wa ushindi
  Ni Mungu wa uweza
 • Ameumba jua na mwezi,
  vinavyong'ara vyote kaumba
  Ameumba radi inayonguruma,
  yenye kutisha yenye kuogofya
 • Ameumba giza na kimya
  akaviumba vilivyo tuli
  Ameumba maji yanayofariji,
  yenye kupoza na kuburudisha
 • Astahili sifa na utukufu,
  Astahili enzi na utawala
  Astahili kusifiwa na kutukuzwa,
  Astahili kusifiwa milele milele
 • Astahili sifa, astahili enzi *2
  Astahili sifa, Astahili sifa na heshima
  Astahili sifa *2 sifa astahilina heshima
 • Kaweka mamlaka zake mikononi mwa watu
  Ni watu wadogo mno kwenye koo duni tu
  Kawapa fimbo yake kuu wamchungie kondoo
  Wakaifanye kazi kwenye shamba lake kuu
 • Ndiye Mungu wa babu abrahamu na wa Isaka
  (Na yeye) Ndiye Mungu wa Yakobo na daudi
  Ni Mungu wa milele
 • Ni Mungu mkuu * 2 ni Mungu wa ushindi
  Ni Mungu mkuu *2 ni Mungu wa uweza
 • {Astahili kusifiwa kutukuzwa milele *2
  Ni Mungu mkuu wa ushindi,
  Ni Mungu mkuu wa uweza
  Ni Mungu Mungu hutenda makuu } * 2
 • Ni Mungu mkuu *3 ni Mungu wa ushindi
  Ni Mungu mkuu *3 ni Bwana wa mabwana

Favorite Catholic Skiza Tunes