Raha ya Mbinguni

Raha ya Mbinguni
Performed bySt. Cecilia Mirerani
AlbumMaajabu ya Mungu
CategoryTafakari
ComposerA. Manota
Views5,423

Raha ya Mbinguni Lyrics

  1. Ngoja nikusimulie ndugu yangu raha ya Mbinguni
    (kwa kweli)
    Mbinguni kuna raha, ni hakika kuna raha } * 2
    {Ni raha (ni raha) mbinguni ni raha ni raha tu
    Mbinguni ni raha,
    ni raha (Mbinguni) ni raha ni raha tu
    Mbinguni ni raha
    Ni raha ni raha ni raha (kweli) mbinguni ni raha}

  2. Huko watu hawafi kamwe - ni raha tu
    Huko hakuna ma-gonjwa
    Huko hawaijui huzuni
    Mbingu ni raha ndugu
  3. Malaika huimba huko
    Wateule husifu huko
    Watakatifu husujudia
    Mbinguni ni raha ndugu
  4. Kila nyumba ni kwake Mungu
    Ndiyo yerusalem mpya
    Huko yuko mama maria
    Mbinguni ni raha ndugu
  5. Tukitubu tutaingia
    Tutamwona mwokozi Yesu
    Tutasifu milele yote
    Mbinguni ni raha ndugu