Siri ya Mafanikio Lyrics

SIRI YA MAFANIKIO

 1. Nikateleza nikatapatapa,
  sauti ile ikanirudia tena
  Ikanambia usiwe na hofu,
  inua macho yako kwenye mti huu (na kisha)

  Tazama tundu hili takatifu la neema
  Kwenye moyo uliojaa pendo
  Na ndilo siri ya mafanikio ya maisha
  Ya furaha na amani ya kweli (aleluya)
  Wa Yesu umefunuliwa moyo huo
  Nauona uko wazi moyo ( tukufu)
  Unanimiminia neema moyo huo
  Uko wazi uko wazi moyo

 2. Ulipochomwa kwa chuma kigumu,
  na ni ugumu ule wa mioyo yetu
  Ukatujibu kwa kumwaga maji,
  maji laini nayo damu ya sadaka (lakini)
 3. Hauchukii hauna kisasi,
  moyo mpole mwema na mnyenyekevu
  Shida na tabu tukiukabidhi,
  unachotoa ni neema na ushindi
 4. Mahangaiko na kumaka kwetu,
  tuupelekee moyo wake Yesu
  Tutafurahi tutafanikiwa,
  damu na maji yake yatatutakasa (lakini)
 5. Ili daima atukuzwe Baba,
  na mwana atukuzwe Roho Mtakatifu
  Ilivyokuwa toka kule mwanzo,
  sasa na siku zote daima milele (amina)
Siri ya Mafanikio
CHOIRBMT Ledochowska K/Ndege Dodoma
ALBUMDawa ya Uzima
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYG Major
TIME SIGNATURE12
16
SOURCESumbawanga
NOTES Open PDF
 • Comments