Ukiwaona Kama Watu

Ukiwaona Kama Watu
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumRamani ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerE. F. Jissu

Ukiwaona Kama Watu Lyrics

Ukiwaona kama watu - hao, kama watu
Kumbe ndani ni mbwa mwitu - hao, mbwa mwitu
Wamejivika mavazi ya kondoo * 4

 1. Sura zao zinavutia machoni pa watu
  Na kuonekana wao ni wa maana kwa watu
  Matapeli wakuu ni wao, ni wao, ni wao wanadamu
  Wala rushwa wakuu ni wao, ni wao, ni wao wanadamu
 2. Vinywa vyao hunena maneno matamu kwa watu
  Na kuonekana wenye hekima nyingi kwa watu
  Kumbe ndani hao ni wachafu (wachafu *2) wanadamu
  Wanadhani Mungu hawaoni (wachafu *3) wanadamu
 3. Kwa ushirikina wao ni viongozi hodari
  Hujisifia kwa mambo yao maovu kwa watu
  Kumbe wanajilisha upepo mchafu
  Kwa hivyo unayo hii (nafasi *2) kwa Mungu mwanadamu
 4. Ufisadi uso na mfano ni wao ni wao
  Ukiwaona wala huwezi dhania ni wao
  Kweli ndugu inasikitisha, ni wao, ni wao wanadamu
  Hawamuogopi hata Mungu ni wao ni wao wanadamu
 5. Nyumba za ibada hawakosekani, kwa kweli
  Na nyadhifa pia wanajitwalia aibu
  Mnamdhalilisha Mungu, Mungu, Mungu, wanadamu
  Elewa Mungu anakuona, kuona, kuona, mwanadamu