Duka la Shetani

Duka la Shetani
Alt TitleUsipange Foleni
ChoirSt. Veronica Kariakor Dar-es-salaam
AlbumKama Nyuki
CategoryTafakari
ComposerVictor Aloyce Murishiwa

Duka la Shetani Lyrics

Usipange foleni kwenye duka la shetani
Utauziwa dhambi faida yake mauti
Nenda ukajipange dukani kwa Bwana Yesu
Utapata kibali cha kuingia mbinguni

 1. Enyi wavuta bangi, na madawa ya kulevya
  Mbona mmejipanga katika duka la shetani
 2. Na ninyi wala rushwa, makahaba na wachawi
  Mbona mmejipanga katika duka la shetani
 3. Duka lake shetani limejaa vitu vingi
  Tena vyapendeza sana na kuuvutia moyo
 4. Ramani ya mbinguni nenda kwake Yesu
  Ramani ya kuzimu shetani ndiye mchoraji
 5. Mnaofunga ndoa katika jinsia moja
  Nanyi mmejipanga katika duka la shetani
 6. Mavazi ya aibu dada zetu mwajivika
  Mnaita vimini shetani anachekelea