Ulimi ni Uovu

Ulimi ni Uovu
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumRamani ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerO. Okwako

Ulimi ni Uovu Lyrics

Ni nani awezaye kuufuga ulimi, ulimi, ulimi *2
Ulimi ni uovu huu, ulimi unaleta ugombanishi
{ Ulimi ulimi ulimi, ulimi ulimi ulimi
Ulimi ulimi ulimi, ulimi kiungo kidogo
Lakini una sumu kali iletayo mauti } * 2

 1. Ulimi ni kitu kiovu wala hakiwezi kutawalika
  Lakini kimejaa uovu, uovu uletao mauti
 2. Tazama tunamshukuru Muumba kwa kutumia ulimi
  Na tena twatumia ulimi huo kuwalaani wenzetu
 3. Tazama wote tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu
  Maneno ya laana kusifu yatoka kweli kinywa kimoja

  //hitimisho//

  Je chemichemi moja yaweza kutoa maji matamu
  Je mti wa mpini waweza kuzaa zeituni
  Wala chemichemi ya maji ya chumvi kutoa maji matamu
  Je chemichemi moja yaweza kutoa maji machungu
  Je mti wa zabibu waweza zaa tunda la mpini
  Wala chemichemi ya maji ya chumvi kutoa maji matamu