Nyumba ya Roho

Nyumba ya Roho
Performed bySt. Kizito Makuburi
AlbumNyumba ya Roho
CategoryRoho Mtakatifu (Pentecoste)
ComposerCharles Ruta
Views9,395

Nyumba ya Roho Lyrics

  1. Mungu wangu nikujue mimi, Mungu wangu nikupende
    Mungu nikutumikie, kisha niurithi ufalme Mbinguni * 2
    (wewe) roho umenipa ee, (kisha) ukaihifadhi vizuri
    (yaani) ndani ya mwili ee (kwani) mwili ni nyumba ya rho

  2. Ndiwe mungu peke yako, wa kuabudiwa ni wewe
    Nishike kitakatifu siku hiyo siku yako
    nisilitaje kabisa bure jina lako Mwenyezi
    Ulimi wa mwili wangu usiiponze roho yangu
  3. Niwaheshimu wazazi, ili nisiwasononeshe
    Uhai wa binadamu niuthamini yani nisiuue
    Kuiba nijiepushe, kusema uwongo niache
    Mwili wangu usizini ndipo roho yangu itapona
  4. Niepuke kutamani yote yasiyo mali yangu
    Naye mwanamke asiye mke wangu yani sio wangu
    Hapo ndipo nitakuwa nimeutumia vizuri
    Mwili ulioiumbia roho ifike Mbinguni juu