Uko Juu Lyrics

UKO JUU

@ Bernard Mukasa

 1. Hufanani nasi, unang'ara na tena una enzi, una utukufu
  Umepita zote, sifa tunazokutolea sisi, nao malaika oho

  Wewe uko juu umetukuka na tunakuinua kwa nyimbo zetu hizi

 2. Walikuimbia, baba zetu lakini hazikwisha, sifa zako wewe
  Na watakatifu, wanaimba na hazimaliziki, tenzi hazitoshi oho
 3. Mimea ya nchi, yaeleza inapopukutika, kuhifadhi maji
  Kwamba wewe Bwana, hupungui unajua kuumba, hupitiwi neno oho
 4. Kinyonga mdogo, anageuka rangi kujilinda, bila ya bunduki.
  Anafafanua, umakini ndani ya kazi yako, isiyo dosari oho
 5. Na uhimidiwe, wewe Baba yaani ndiwe Mwana, Roho Mtukufu,
  Ulivyotukuzwa, enzi zile sasa hata milele, utukuzwe pote oho
Uko Juu
COMPOSERBernard Mukasa
CATEGORYTafakari
 • Comments