Mlipuko wa Sifa Lyrics

MLIPUKO WA SIFA

@ Bernard Mukasa

 1. [ s ] Zikumbukeni njia alizowapitisha
  [ w ] Amewapenda amewang`ang`ania ninyi
  Hajaufumba ukope wake hata mara moja
  Amewapenda amewang`ang`ania ninyi
  Hajazifumbua mbawa zake msilowe mvua
  Amewapenda amewang`ang`ania ah

  Lipua pu! pu! pu pu pu! puu!
  Lipua sifa - sifa kwa Mungu Baba lipua
  Lipua shangwe- sifa kwa Mungu Baba lipua
  Lipua tena - sifa kwa Mungu Baba lipua aa
  (amsheni hisia, lipua sifa, inueni mioyo lipua sifa)
  Lipua lipua lipua aa lipua lipua, lipua puu

 2. Kumbuka mlivyokuwa na hali duni kule mwanzo,
  Ni yeye Mungu aliyewabeba
  Mlipopotea njia akawakamata mkono . . .
  Ni yeye Mungu aliyewabeba
  Akawaongoza mpaka kufika mlipo leo . . .
  Ni yeye Mungu aliyewabeba
 3. [ b ] Kusanyikeni wote kwa miluzi na nyimbo tumtukuze,
  Paza sauti zenu piga kelele kumsifu
  Cheza kidogo wote inueni mikono shangilieni.
  Paza sauti zenu piga kelele kumsifu
  Rusha miguu yenu kwa midundo mitamu tumtukuze . . .
  Paza sauti zenu piga kelele kumsifu

  Paza sauti - zenu piga kelele kumsifu
  Nyinyi na nyumba - zenu piga kelele kumsifu
  Na majirani -zenu piga kelele eh
  ~ ~ ~
  Tunampigia aah ngoma tamu
  Tunamchezea aah ngoma tamu kabisa
  Tumpigie - vigelegele makofi *6
Mlipuko wa Sifa
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Yuda Thadei Mbeya
ALBUMMlipuko wa Sifa
CATEGORYEntrance / Mwanzo
MUSIC KEYKEY G
TIME SIGNATURE2/4
NOTES Open PDF
 • Comments