Login | Register

Sauti za Kuimba

Milele Yesu Nitakusifu Lyrics

MILELE YESU NITAKUSIFU

{ Milele ee (Yesu) nitakusifu milele *2
Kwa nyimbo za shangwe nitakusifu milele *2 aleluya } *2

 1. Mwokozi katenda mambo ya ajabu,
  Kaniweka huru amenifungua
  Ni shangwe kubwa kukombolewa *2
 2. Wakati wa shida kanisaidia,
  Ameniondoa ndani ya mitego
  Ni shangwe kubwa kukombolewa *2
 3. Kanihakikisha uzima Mbinguni,
  Kaniondolea hukumu ya dhambi
  Ni shangwe kubwa kukombolewa *2
Milele Yesu Nitakusifu
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments