Rafiki Yangu Njoo Lyrics

RAFIKI YANGU NJOO

@ J. Bahati

 1. Rafiki yangu njoo kaa chini, nisikilize kwa makini
  Rafiki njoo kaa chini ,nikueleze jambo moja aah

  {Kila mtu atalipwa sawasawa na matendo ooh
  Kila mtu atalipwa sawa nayo matendo yake } * 2
 2. Kama uliua kwa upanga, utakufa kwa upanga
  Uliua kwa silaha, utakufa kwa silaha aah
 3. Kama ulikuwa ni mzinzi, utakufa kwa uzinzi
  Ulikuwa mzinifu, utakufa kwa uzinzi iih
 4. Kama ulikuwa mfitini, utalipwa ufitini
  Ulikuwa mfitini, utalipwa ufitini iih
 5. Kama ulikuwa mkarimu, utalipwa ukarimu
  Ulikuwa ni mchoyo, utalipwa sawa na choyo ooh
 6. Kama ulinitendea wema, utalipwa matendo mema
  Ulinitendea baya, utalipwa kwa ubaya aah
Rafiki Yangu Njoo
COMPOSERJ. Bahati
CHOIRSt. Cecilia Isibania
CATEGORYTafakari
 • Comments