Mpeni Bwana Utukufu (B. Mukasa)

Mpeni Bwana Utukufu (B. Mukasa)
Alt TitleSauti Sauti ya Bwana
Performed bySt. Kizito Makuburi
AlbumMungu Yule
CategoryZaburi
ComposerBernard Mukasa
Views6,632

Mpeni Bwana Utukufu (B. Mukasa) Lyrics

  1. Sauti sauti ya Bwana, sauti ya Bwana i juu ya maji
    Bwana yu juu ya maji ya maji mengi

    Mpeni -mpeni Bwana mpeni
    Mpeni -enyi wana wa Mungu
    Mpeni -Mpeni Bwana mpeni
    Mpeni -utukufu na nguvu
    Mpeni -Mpeni Bwana mpeni
    Mpeni -utukufu wa jina lake
    Mpeni -mwabuduni Bwana
    Mpeni -kwa uzuri wa utakatifu
    Bwana atawabariki watu wake kwa amani

  2. Sauti ya Bwana ina nguvu, ina nguvu
    Sauti ya Bwana ina adhama, ina adhama
    Sauti ya Bwana yawazalisha ayala
    Ndani ya hekalu ndani ya hekalu lake
    Wanasema wote, wanasema wote utukufu
  3. Bwana aliketi juu ya gharika (naam)
    Bwana ameketi hali ya mfalme milele