Login | Register

Sauti za Kuimba

Wangu wa Milele Lyrics

WANGU WA MILELE

@ S. Ndibalema

Mpenzi wangu ungana nami, tumshukuru Mungu wetu
Uje tucheze kwa furaha, tumshukuru Mungu wetu
Kwani ile siku tuliyoingojea - iwe tumshukuru Mungu wetu
Mwenyezi ametujalia - iwe, tumshukuru Mungu wetu

 1. Nasema mbele ya wazazi wako (ni wewe)
  Ni wewe niliyekuchagua (ni wewe)
  Nasema mbele ya wazazi wangu, ni we wangu wa moyoni
  Ninatamka mbele za Mungu (ni wewe)
  Mtima wangu nakupatia (ni wewe)
  Nasema mbele ya wazazi wangu, Ni we wo mtima gwange
 2. Unawaacha wazazi wako (ni wewe)
  Mwili mmoja tunakuwa (ni wewe)
  Nami nitakupenda milele, Ni we wangu wa moyoni
  Ninawaacha wazazi wangu (ni wewe)
  Mwili mmoja tunakuwa (ni wewe)
  Nami nitakupenda milele, Ni we wo mtima gwange
 3. Ndi-we mama wa watoto wangu (ni wewe)
  Mwenyezi Mungu kanipatia (ni wewe)
  Karibu kwetu kipenzi changu, ni we wangu wa moyoni
  Ndi-we baba wa watoto wangu (ni wewe)
  Mwenyezi Mungu kanipatia (ni wewe)
  Nakuja kwenu kipenzi changu, Ni we wo mtima gwange
 4. Nawashukuru wazazi wako, umbo zuri wameniletea
  Namshukuru Mwenyezi Mungu, ni we wangu wa moyoni
  Nawashukuru wazazi wako, lulu yangu walinitunzia
  Haki ya Mungu nitakutunza, ni we wo mtima gwange
Wangu wa Milele
COMPOSERS. Ndibalema
CATEGORYHarusi
MUSIC KEYKey D
TIME SIGNATURE4
8
NOTES Open PDF


Kihaya Melody


Kihaya Melody


 • Comments