Washuhuda wa Yesu

Washuhuda wa Yesu
Performed by-
AlbumWashuhuda wa Yesu
CategoryInjili na Miito (Gospel)
ComposerRenatus Rwelamira
Views2,597

Washuhuda wa Yesu Lyrics

  1. Alipopaa mbinguni aliteka mateka,
    Akawapa wanadamu vipawa

    Kwa wengine zawadi yao ilikuwa wawe manabii
    Na kwa wengine wawe wachungaji wainjilisti na walimu

    { Lakini sisi tumetolewa kuwa mitume
    Tuwe washuhuda wa Yesu Kristu } *2

  2. [ s ] Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu
    Hata kazi ya huduma yake Kristu itendeke
    Hata mwili wa Kristu nao ujengwe
  3. Sisi sote tutakapofikia umoja wa imani
    Kumfahamu Mwana wa Mungu na kuwa mtu mkamilifu
    Kimo cha utimilifu, wa Yesu Kristu
  4. Ili tusiwe tena watoto tukitupwa huku na huku
    Na kuchukuliwa kila kila upepo wa elimu
    Tukizifuata njia za udanganyifu