Furaha Hiyo Niliyo Nayo

Furaha Hiyo Niliyo Nayo
ChoirSt. Michael Otiende Lang'ata
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerM. Z. Yohana

Furaha Hiyo Niliyo Nayo Lyrics


 1. Furaha hiyo niliyo nayo yatoka kwa Mungu *2
  {Ndiye Baba (baba), ninayemtumaini (baba)
  Kwenye maisha yangu, Yeye ndiye kimbilio} *2 Baba

 2. Sina budi kumshangilia Mungu
  Baba kwa huruma yake na wema wake
  Mema mengi aliyonitend`a mimi
  Sina budi kushukuru asante Baba
 3. Yeye ndiye tumaini langu mimi
  Ndiye msaada wangu na wokovu wangu
  Bila Mungu mimi siwezi chochote
  Sina ujanja wowote ni ubatili
 4. Ni wangapi, walimpuuza Mungu
  Kwa kukiuka sheria wakapata fimbo
  Wakarudi, wakamlilia Mungu,
  Kuomba huruma yake, akawasamehe
 5. Nawe ndugu kujiona we mdhambi
  Mungu anakutafuta urudi kwake
  Nenda hima ukatubu dhambi zako,
  Ukaipate furaha iliyo ya kweli