- Bwana u sehemu yangu, rafiki yangu wewe
Katika safari yangu, tatembea na wewe
Pamoja na wewe, pamoja na Wewe
Katika safari yangu, tatembea na wewe.
- Mali hapa sikutaka, ili niheshimiwe,
Na yanikute mashaka, sawasawa na wewe
Pamoja na wewe, pamoja na wewe
Heri nikute mashaka sawasawa na wewe.
- Niongoze safarini Mbele unichukue
Mlangoni mwa Mbinguni, niingie na wewe
Pamoja na wewe, pamoja na wewe
Mlangoni mwa Mbinguni, niingie na wewe
|
|
|