Msamaha ni Maua

Msamaha ni Maua
Alt TitleNarudi zangu Mimi
Performed byBMT Ledochowska K/Ndege Dodoma
AlbumKimbunga
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa
Views8,577

Msamaha ni Maua Lyrics

  1. Narudi zangu mimi kwa upatanisho
    Narudi kwa amani turudiane (aiyo)
    Niliyokukosea unisamehe
    Na uliyonikosea nimekusamehe ndugu yangu

    Narudi zangu mimi kwa upatanisho (ninatafuta amani)
    Narudi kwa amani turudiane (yelele)
    Niliyokukosea unisamehe (na)
    Uliyonikosea nimekusamehe ndugu yangu

  2. Ubinadamu wetu ulituangusha
    tukajeruhiana mioyo yetu (aiyeiye)
    Lakini leo wangu, tufarijiane,
    tuyaache ya nyuma sasa tuanze upya kabisa
  3. Tulipokwaruzana, tulijichafua,
    Tukampa jeuri yule muovu (aiyeiye)
    Tukipatana leo ataaibika
    Haya tumuaibishe sasa tuanze upya kabisa
  4. Nipe mkono wako tukumbatiane
    Jamii ijifunze kutoka kwetu (aiyeiye)
    Sogeza shavu Basi na tunusiane;
    Busu lenye amani (sasa) tuanze upya kabisa.

    Kusameheana kunamleta Yesu katikati ya watu
    Kusamehe ni maua
    Kunapumzisha kunalegeza mwili kunafungua roho
    kusamehe ni maua
    Inapendeza sana msamaha ni maua
    Inavutia sana msamha ni maua
    Inapamba nafsi msamaha ni maua
    Inafungua mbingu msamaha ni maua
Recorded by several Tanzanian choirs including * Kwaya ya Mwenye Maria Theresa, Ledowchoska, Parokia ya Uwanja wa Ndege Dodoma Tanzania * Kwaya ya Mt. Francisco Kwa Ngulelo Arusha and others