Utanisahau Kabisa Mpaka Lini

Utanisahau Kabisa Mpaka Lini
Alt TitleEe Mwenyezi Mungu
ChoirMaria Mt Mama wa Mungu Musoma
AlbumMatumaini ya Safari
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerMarcus Mtinga

Utanisahau Kabisa Mpaka Lini Lyrics

 1. Ee Mwenyezi Mungu utanisahau kabisa mpaka lini?
  Utauficha uso wako mbali nami mpaka lini Mungu wangu?
 2. Roho na mwili wangu vitakuwa na wasiwasi mpaka lini?
  Na masikitiko siku hata siku sina raha maishani
 3. Bwana nimelia sana, mchana uko wapi unifadhili
  Na usiku usingizi sipati nakesha nikiwaza
 4. Nimedhoofika sana fimbo kila siku nachapwa nimekonda
  Sina pa kukimbilia njia zote zimelindwa niende wapi
 5. Maadui zangu ni wengi, njaa magonjwa ya hatari na ajali
  Vita vimepamba moto dunia yote ona Bwana ninavyotishwa
 6. Ndugu na rafiki zangu wametoweka siwaoni wako wapi
  Kama wako kwako Bwana nambie nami nijaribu kuwafuata
 7. Yesu wangu u Mungu wangu njoo haraka nakuita njoo Bwana
  Mwanao nateseka sijiwezi mimi ninaomba msaada wako
 8. Ninainua mikono taabu mateso maumivu yangu yote
  Ninakukabidhi wana yapokee Mwokozi naomba usinitype