Yesu Wangu Niokoe

Yesu Wangu Niokoe
ChoirSt. Maurus Kurasini
AlbumHubirini Kwa Kuimba
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerA. K. C. Singombe
SourceTanzania
Musical Notes
Time Signature3
8
Music KeyC Major
NotesOpen PDF

Yesu Wangu Niokoe Lyrics

Yesu wangu niokoe,
{ Ulimwegu nilimo ni wa mateso
Nishike mkono wangu Bwana niokoe
Ulikuja duniani kwa wadhambi,
Nitakase kwa damuyo Bwana nitakate
Bwana nakukimbilia } *2

 1. Nionyeshe uso wako uso mkunjufu, nisamehe dhambi,
  Nakusihi Mwokozi, Bwana unisikie
 2. Nimefanana na mwana mwana mpotevu, dhiki na karaha
  Vimenisonga sana Bwana unisikie
 3. Wewe ndiwe ngome yangu ngao yangu tumaini langu
  Ninakutegemea Bwana unisikie
 4. Roho yangu mwili wangu vyote ni vyako ndivyo ulivyoumba
  Viimarishe Bwana, Bwana unisikie
 5. Mungu Baba Mungu mwamba Mungu mkombozi
  Mungu wa mapaji, Utatu Mtakatifu usifiwe milele