Login | Register

Sauti za Kuimba

Mimi Ni Mtumishi Lyrics

MIMI NI MTUMISHI

@ Fr. G. F. Kayeta

{ Mimi ni mtumishi wake Bwana, nitendewe ulivyonena *2
Nitendewe ulivyonena, mimi ni mtumishi wa Bwana } *3

 1. Salamu uliyejaa neema, Bwana yu pamoja nawe
  Usiogope Maria, Mungu kakupendelea
 2. Tazama utapata mimba utazaa mwana, utamwita jina Yesu,
  Huyu atakuwa mkuu, ataitwa mwana wa aliye juu
 3. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi, cha Baba yeke Daudi
  Ataitawala nyumba ya Yakobo hata milele
  Ufalme wake hautakuwa na mwisho
Mimi Ni Mtumishi
COMPOSERFr. G. F. Kayeta
CHOIRShirikisho la Kwaya Katoliki Dsm (Shikwaka)
ALBUMKaribu Tanzania
CATEGORYBikira Maria
 • Comments