Simba wa Israeli

Simba wa Israeli
Performed by-
AlbumBwana Kafufuka
CategoryTBA
ComposerBernard Mukasa
Views3,302

Simba wa Israeli Lyrics

  1. { Simba wa Israeli anaunguruma,
    Mbingu za shangwe zinatikisika, zinarukaruka
    Ulimwengu wa burudani unatetemeka
    Miamba mikubwa mikubwa inasambaratika } *2
    {
    /s/
    Ni shangwe na vigelegele, nderemo chereko vifijo, kwa makofi
    Shangilieni, Bwana yesu amefufuka
    Manowari ya ukombozi imetia nanga

    /a/
    Ni shangwe na vigelegele, ni nderemo na vifijo makofi ya shangwe
    Kwa furaha Mwana wa Mungu amefufuka
    Manowari ya ukombozi imetia nanga

    /t/
    Ni shangwe, vigelegele, nderemo na vifijo
    Waumini pigeni makofi, Mfalme Yesu amefufuka
    Manowari ya ukombozi imetia nanga

    /b/
    Ni shangwe na vigelegele, nderemo chereko vifijo
    shangwe shangwe, ukombozi Kristu Yesu amefufuka
    ya ukombozi manowari imetia nanga

    } *2

  2. [a] Aliyekufa mtini bila kosa,
    /a/ (akakubali) kuungama na dhambi zetu, amefufuka tumetakasika milele
    /s/ akakubali kuyatubu makosa yetu, ameshinda tumetakasika milele
  3. Hatima ya nguvu zote za shetani, (imetangazwa)
    umeangusha utawala wa mwovu na tumwimbie (wote) aleluya
  4. Utakatifu wa mwanzo, tulioupoteza kwa dhambi
    Hii Leo, ameurudisha
    hesabu ya watoto wa Mungu upya tumerudishiwa
  5. Aliye sadaka ya agano jipya
    Amedhihirisha utukufu wake machoni petu
    Astahili kutukuzwa kwa sauti kuu