Ee Bwana Nifundishe Kupenda Lyrics

EE BWANA NIFUNDISHE KUPENDA

@ Bernard Mukasa

Ee Bwana nifundishe kupenda, ee Bwana nifundishe kutumikia
Ee Bwana nifundishe (kuwajua wenzangu ee) Ee Bwana nifundishe kutumikia

 1. Nifanye juhudi kuwajua watu, kusudi nizifahamu shida zao
  Nisiwape kazi kubwa kutafuta njia ya kunieleza shida zao
  Nisiwe mwenye haraka kuwachoka, niliowasaidia mara nyingi
  Nijue kusaidia ni safari, iliyo na milima mingi na miiba
 2. Nijue kuwatetea wadhaifu, wasipoteze thamani nikiona
  Maana hawakuchagua hali yao. Wamekuwa hivyo kusudi utukuzwe
  Nijibidiishe daima kutafuta, kuwasiliana na jamaa zetu
  Kwa kuwa mahusiano ni gharama, hayawezi kuwepo bila jitihada
 3. Maana nikishajua kupenda, na nikazingatia kutumikia
  Kilicho nileta hapa duniani, kitakuwa kimetia niondoke
Ee Bwana Nifundishe Kupenda
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Gregory kwa Mrombo
ALBUMKanyaga Twende
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYG Major
TIME SIGNATURE6
16
NOTES Open PDF
 • Comments