Ninakushukuru Bwana Lyrics

NINAKUSHUKURU BWANA

@ J. Mugangos

 • Ninakushukuru Bwana, ninakushukuru Bwana
  Kwa mema unayonijalia ninakushukuru
  Ninakushukuru Bwana
  mimi ninakushukuru Bwana mimi ninakushukuru Bwana
  Ninakushukuru Bwana
  mimi ninakushukuru Bwana mimi ninakushukuru Bwana
 • Nina kila sababu ya kukushukuru Bwana
  (Tena) Tena inanipasa nitoe shukrani zangu,
  Kwako wewe Muumba wangu muumba wangu, ewe Mungu wangu
 • {Ninatazama jinsi nilivyo mimi,
  ni wewe Bwana uliyeniumba mimi (Bwana)
  Ukanipa uzima, ukanipa uzima, pia na akili } * 2
 • Na tazama na pia vitu vyote nilivyo navyo
  Nimevipata kutoka kwako Bwana Mungu wangu
  Kwa nini nisishukuru, kwa nini?
  Kwa nini nisikushukuru Bwana
  Kwa nini nisikushukuru Bwana
  Kwa nini nisikushukuru Bwana Muumba wangu
  (Yanipasa) Yanipasa nikushukuru
 • { Ninakushukuru kwa moyo wangu wote
  Ninakushukuru Mungu wangu
  Ninakushukuru Mungu wangu
  Ninakushukuru Mungu wangu kwa moyo wangu wote } * 2
 • Ninakusihi ewe Bwana Mungu wangu
  uzipokee shukrani zangu
  Ingawaje shukrani zangu hazilingani na wema wako kwangu, ee Mungu wangu
 • Ninafahamu Bwana unanipenda, ingawaje
  Waujua udhaifu wangu na mawazo yangu yote ya kila siku
  Na maneno na matendo yangu yote
 • Ninajiuliza nikushukuru jinsi gani Mungu wangu
  Nitakuimbia wimbo wa sifa
  Wimbo ule ulio bora wimbo wa shukrani, wa shukrani
  Niyatangaze matendo yako makuu
  Na sifa zako na wema wako wakati wote
  Na pia mahali pote
 • Nitalitangaza Neno lako kwa watu wote, wakuheshimu wakufuate wewe
  Ninakuomba uniimarishe pia unilinde, ili nikufuate wewe daima na daima
  nami nitakushukuru siku zote za maisha yangu nisadie Bwana
 • Ninakushukuru Bwana, ninakushukuru Bwana
  Kwa mema unayonijalia ninakushukuru
  Ninakushukuru Bwana, ninakushukuru Bwana
  Kwa mema unayonijalia ninakushukuru
 • Ninatoa asante kwako Bwana Mungu wangu
  Asante, asante, asante,
  Ninatoa asante kwako Bwana Mungu wangu
  Asante, asante, asante,
 • a-asante (asante), a-asante (asante) , a-asante (asante asante),
  asante asante asante (asante)
 • a-asante (asante), a-asante (asante) , a-asante (asante asante),
  asante Mungu Baba asante
Ninakushukuru Bwana
ALT TITLEJ. Mugangos
COMPOSERJ. Mugangos
ALBUMHaya Tazameni (Vol 21)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments