Login | Register

Sauti za Kuimba

Wakati Sasa Umefika Lyrics

WAKATI SASA UMEFIKA

Wakati sasa umefika, wa kutoa sadaka
Amka ndugu tupeleke, sadaka zetu kwake
Ni mema mengi sana kila siku anatugawia
Lakini tunshindwa kumshukuru Mungu Baba
Twendeni kwa pamoja tupeleke sadaka zetu
Tutoe kwa upendo Mungu Baba atapokea

 1. Ee ndugu fikiria maisha yako yote
  Tangu kuumbwa kwako na bado unaishi
  Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
 2. Usiku na mchana hachoki kutulinda
  Tukiwa na safari ajali aepusha
  Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
 3. Uwezo wako wote umepewa na Mungu
  Na kazi ufanyazo Mungu amebariki
  Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
 4. Mapato yako yote yanatoka kwa Bwana
  Ingawa ni kidogo Bwana atapokea
  Mshukuru Mungu Baba kwa kutoa sadaka
Wakati Sasa Umefika
CATEGORYOffertory/Sadaka
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments