Ufalme wa Mbinguni

Ufalme wa Mbinguni
Choir-
CategoryMafundisho ya Yesu
ComposerJoseph Makoye

Ufalme wa Mbinguni Lyrics

Ufalme wa Mbinguni umefanana na mtu
aliyepanda mbegu njema katika konde lake
Lakini watu walipolala akaja adui yake
Akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake

Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa
yakaonekana na magugu
Watumwa wa mwenye nyumba wakamwambia
Bwana hukupanda mbegu njema katika konde lako
Limepata wapi basi magugu

Akawaambia,
Adui ndiye aliyetenda hivi
Watumwa wakasema,
Basi wataka twende tukayakusanye
Naye akasema,
Na msije mkakusanya magugu, na kuzitwaa ngano pamoja nayo

Viacheni vyote vikue mpaka wakati wa mavuno
Na wakati wa mavuno, nitawambia wavunao
Yakusanye kwanza magugu, myafunge machicha machicha,
mkayachome
Bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442