Naye Autengenezaye Mwenendo Lyrics

NAYE AUTENGENEZAYE MWENENDO

Naye autengenezaye mwenendo wake mwenyewe
Nitamuonyesha nitamuonyesha wokovu wa Mungu
Naye autengenezaye mwenendo wake mwenyewe
Nitamuonyesha nitamuonyesha wokovu wa Mungu

 1. Mungu Mungu mwana amenena ameiita nchi
  Toka mawio ya jua hata machweo yake
  Sitakukemea kwa ajili dhabihu zako
  Na kafara zako ziko mbele yangu daima
 2. Kama ningekuwa na njaa singekuambia
  Maana ulimwengu ni wangu navyo viujazavyo
  Je nile nyama nyama ya mafahari
  au ninywe ninywe damu ninywe damu ya mbuzi
 3. Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru
  Mtimizie aliye juu nadhiri zake
  Ukaniite siku siku ya mateso
  Nitakuokoa nawewe utanitukuza
Naye Autengenezaye Mwenendo
ALBUMKwa Wingi wa Fadhili
CATEGORYZaburi
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments