Tunu Yetu Lyrics

TUNU YETU

Pema huwa pema hujapopema, ukishapema si pema tena
Edeni ilikuwa haki yetu, tukaasi tukatupwa pipani
Utulivu na amani Tanzania ni silaha,
tudumishe amani yetu tunu yetu -
Utulivu na amani Tanzania ni silaha,
tudumishe amani yetu tunu yetu jema

 1. Tumepewa kwa upendeleo, utulivu Tanzania ni tunu
  Hatukuinunua kwa fedha, amani ni namba moja (amani)
 2. Madaraka yasitudanganye, utulivu Tanzania ni tunu
  Utajiri usituchanganye, amani ni namba moja (amani)
 3. Tunapokosoana wapendwa, utulivu Tanzania ni tunu
  Tunapoelezana ukweli, amani ni namba moja (amani)
 4. Kwenye shibe na kwenye furaha, utulivu Tanzania ni tunu
  Kwenye njaa na kwenye huzuni, amani ni namba moja (amani)
 5. Tukumbuke ametupa bure, utulivu Tanzania ni tunu
  Tukimwuzi ataiondoa, amani ni namba moja (amani)

  Tuitunze kama yai, tunu yetu jema
  Tuilee na tuipambe, tunu yetu jema
  Tuitunze itutunze, tunu yetu jema
  Tuilishe na tuinyweshe, tunu yetu jema

  Tunu yetu jema, tunu yetu jema
  Tunu yetu jema ee, tunu yetu jema
  Tuitunze siku zote, tunu yetu jema
Tunu Yetu
ALT TITLEUtulivu na Amani
ALBUMMilele Milele Nitakusifu
CATEGORYTafakari
 • Comments