Hii ni Sauti

Hii ni Sauti
Performed byKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
AlbumMilele Milele Nitakusifu
CategoryMajilio (Advent)
ComposerE. F. Jissu
Views5,565

Hii ni Sauti Lyrics

  1. Hii ni sauti ya mtu yule, aliaye kutoka nyikani * 2

    Itengezeni njia ya Bwana,yanyoosheni mapito yake * 2
    Na wote wenye mwili watauona, wokovu wa Mungu aleluya * 2

  2. Haya ng'oeni magugu yote, tusafishe tusafishe
    Haya ng'oeni na mizizi yake, tusafishe tusafishe
    {Tusaishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
    Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe}
  3. Tuichimbeni mizizi ya rushwa, tusafishe tusafishe
    Tuyafukieni mashimo ya rushwa, tusafishe tusafishe
    Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
    Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe
  4. Tujaze kifusi penye ubinafsi, tusafishe tusafishe
    Tujenge upendo kwa jamii yote, tusafishe tusafishe
    Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
    Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe
  5. Penye fitina tumwage Molami, tusafishe tusafishe
    Penye majungu tumwage Molami, tusafishe tusafishe
    Tusafishe bila ya kinyongo, ndugu zangu tusafishe
    Tusafishe kwa moyo mmoja, ndugu zangu tusafishe
  6. Tuzisafisheni nyumba za wachawi, tusafishe tusafishe
    Tuzisafisheni kwa jina la Mungu, tusafishe tusafishe
    (ii) Tusafisheni kwa imani, ndugu zangu tusafishe
    Tusafishe siku ile yaja, ndugu zangu tusafishe
  7. Tuing'oeni mizizi ya vita, tusafishe tusafishe
    Tupalilie shamba la upedo, tusafishe tusafishe
    (ii) Sisi sote ni watoto wa Mungu, ndugu zangu tupendane,
    Sisi sote baba yetu mmoja, ndugu zangu tupendane.