Nikurudishie Nini Bwana

Nikurudishie Nini Bwana
Performed bySt. Monica Lower Kabete Campus UoN
AlbumUwe Nami Bwana
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerEvans Kibet
Views5,187

Nikurudishie Nini Bwana Lyrics

  1. Nikurudishie nini - Mungu nirudishe nini
    Mema mengi umenitendea, na mazuri mbalimbali

    Sio afya (afya), sio mali (mali)
    Si elimu (kweli) sio nyumba (Bwana)
    Ninajiuliza kweli nirudishe nini x2

  2. Kweli umenibariki katika maisha yangu,
    Bwana mimi hivi nilivyo mbona nisikushukuru.
  3. Tazama bomani ng'ombe, mbuzi nao kuku pia,
    Wa kutaga wa kuuza, kweli nimebarikiwa.
  4. Mvua inarutubisha, mimea inasitawi,
    Maua ya kupendeza, aa yapendeza.
  5. Watoto umenijalia, wana pia wajukuu,
    Moyoni nina furaha, aa furaha tele.